CHAD, ambayo Majuzi ililtandikwa Bao 1-0 na Tanzania wakiwa kwao huko Mjini N’Djamena, Leo wametangaza kujitoa Mashindano haya ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, na kulivuruga Kundi G ambalo pia wapo Nigeria na Egypt.
Kujitoa kwa Chad, ambao Kesho Jumatatu Machi 28 walipaswa kushuka Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kurudiana na Tanzania, kulitangazwa hii Leo na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Chad, Moctar Mahamoud, ambae alisema hawana Fedha na hivyo wameshindwa kuisafirisha Timu kwenda Dar es Salaam.
Kujitoa kwa Chad kumeacha Kundi G liwe na Mechi moja tu Wiki huu hapo Jumanne huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria wakati Egypt ikicheza tena na Nigeria baada ya Juzi kutoka Sare 1-1 huko Kaduna.
Kwa mujibu wa Kanuni za CAF, Mechi za Chad za Kundi G sasa zinafutwa na kuiacha Egypt ikiwa kileleni ikiwa na Pointi 4, ikifuata Nigeria Pointi 2 na Tanzania Pointi 1.
AFCON 2017
MAKUNDI:
KUNDI A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
KUNDI B: Madagascar, DRC, Angola, CAR
KUNDI C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
KUNDI D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
KUNDI E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
KUNDI G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
KUNDI H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
KUNDI I: Cote d’Ivoire, Sudan, Sierra Leone, Gabon
KUNDI J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Seychelles
KUNDI K: Senegal, Niger, Nambia, Burundi
KUNDI L: Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland
KUNDI M: Cameroon, South Africa, Gambia, Mauritania
MFUMO:
-Makundi yapo 13 ambapo 12 yana Timu 4 na moja lina Timu 3 lakini Wenyeji Gabon, ambao wanafuzu moja kwa koja kucheza Fainali, wamechomekwa Kundi hilo [KUNDI I] ambapo Mechi zao ni za Kirafiki tu.
-Mshindi wa kila Kundi [Washindi 13] na Timu 2 zitakazomaliza Nafasi za Pili Bora zitatinga Fainali kuungana na Wenyeji Gabon na kufanya Jumla ya Timu 16.
AFCON 2017
RATIBA
Mechi za Makundi
Jumapili Machi 27
Mozambique v Ghana [Estádio Nacional do Zimpeto] 17:00
Kenya v Guinea-Bissau [Nyayo National Stadium] 17:00
Congo v Zambia [Stade Alphonse Massamba-Débat] 18:30
Jumatatu Machi 28
Liberia v Djibouti
Togo v Tunisia
Central African Republic v Madagascar
Benin v South Sudan
Equatorial Guinea v Mali
Botswana v Comoros
Uganda v Burkina Faso
Libya v Sao Tome
Morocco v Cape Verde
Tanzania v Chad [MECHI HAIPO, CHAD WAMEJITOA]
Rwanda v Mauritius
Sierra Leone v Gabon
Sudan v Ivory Coast
Lesotho v Seychelles
Ethiopia v Algeria
Namibia v Burundi
Niger v Senegal
Malawi v Guinea
Gambia v Mauritania
Zimbabwe v Swaziland [National Sports Stadium] 16:00
Jumanne Machi 29
Angola v Congo DR [Estádio 11 de Novembro] 20:00
Egypt v Nigeria [Borg El Arab Stadium] 21:00
South Africa v Cameroon [Moses Mabhida Stadium] 21:00
MSIMAMO WA MAKUNDI:
NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South
0 comments:
Post a Comment