MAN UNITED: DE GEA NI BORA 2016, SMALLING, MARTIAL, CAMERON, RASHFORD WAZOA TUZO!



DEGEA-BORA16












KIPA wa Manchester United David de Gea ameweka Historia ya kuwa Mchezaji wa kwanza Klabuni hapo kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka mara 3 mfululizo baada ya Jana kutunukiwa ile ya Mwaka 2016.
Kwenye Hafla maalum ya kutunuku Tuzo za Man United iliyofanyika Jana Usiku, De Gea alipewa Tuzo ya Sir Bobby Charlton huku Wachezaji wengine kadhaa wakizoa Tuzo mbalimbali.

UZO ZA MAN UNITED 2016:-MCHEZAJI BORA: David De Gea-MCHEZAJI BORA KWA WACHEZAJI: Chris Smalling-GOLI BORA: Anthony Martial (Kwa Goli lake la kwanza kabisa aliloifungia Man United ikiifunga Liverpool Old Trafford)-MCHEZAJI BORA U21: Cameron Borthwick-Jackson-MCHEZAJI BORA U18: Marcus Rashford
SMALLING-BORA16Wakati wa Hafla hiyo, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amedai yeye ni mmoja wa 'Mameneja Bora Duniani.'Pia Van Gaal aliwaponda Wanahabari kwa kumsakama na kuhoji kuhusu kibarua chake kila wakati.Van Gaal alieleza: "Kwa kuandika kwa Miezi 6 mfululizo kuwa nimefukuzwa mie naweza kuhimili lakini ni ngumu kwa Wachezaji wangu!"Aliongeza: "Mie sipo kama Wanahabari wanavyochukulia, mimi nina kiburi kwani ni mmoja wa Mameneja Bora Duniani!"
Share on Google Plus

About darubini

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment